Aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao, amefariki dunia.
Kifo chake kimethibitishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Paul Chacha aliyeeleza kuwa Kamanda Abwao amefikwa na umauti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, akipatiwa matibabu.
