
Na Paul Kayanda, Geita
MGODI wa Dhahabu uliopo katika kijiji cha Mwamakiliga, kata ya Izunya, wilayani Nyang'hwale, Mkoani Geita umeelezwa kusaidia zaidi ya wananchi 6000 kupata ajira mbalimbali katika mgodi huo.
Akizungumza na jopo la waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vilivyotembelea mgodi huo Ili kujionea shughuli hizo, Meneja msaidizi Mashaka Kulwa Chitela amesema wananchi wa kada mbalimbali kutoka ndani ya wilaya ya Nyang'hwale na nje ya wilaya hiyo wanaendelea kunufaika na ajira kwa kufanya shughuli mbalimbali zinazopatikana mgodini hapa.
Aidha amesema kuwa mgodi huo unazalisha mawe Kwa wingi ambapo Kwa wiki ni zaidi ya mifuko ya viroba vya mawe 30,000.
Akizungumzia ajira hizo amesema kuwa wananchi hao wanajishughulisha na shughuli za uchimbaji, uokotaji wa mawe ya dhahabu(maarufu ukwale), biashara ya mitambo ya kusaga mawe (crushers), ubebaji wa mifuko ya mawe, boda boda, mama lishe, mabinti kufanya shughuli ndodondogo zilizopo katikà ofisi za mgodi, biashara za ujasiriamali, Nyumba za kupangisha, maduka, pamoja na shughuli yingine kwa kuzingati Sheria za tume ya Madini na utaratibu uliowekwa na Ofisi ya Mkoa wa kimadini Mbogwe.
"Uwepo wa mgodi huu ni kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira, hapa kuna umati wa zaidi ya watu 6000 wanaojipatia riziki zao za Kila siku. Wapo wachimbaji, wapo kina mama wa ukwale, makago wanaobeba na kupakia mifuko ya mawe, boda boda, mama lishe, wenye Nyumba za kulala wageni, maduka na wajasirimali wadogo wanaochuuza na kupambana kupitia wachimbaji", anasema Chitela Meneja msaidizi wa Mwamakiliga Gold Mining.
Aliongeza kuwa, pia mgodi umetengeneza ajira za uhakika zaidi ya watu 100 katika kada za ukaguzi, ulinzi, ulipuaji na uhudumu wa ofisini na kwamba matumani makubwa ya mgodi ni kuzalisha ajira Nyingi zaidi iwapo serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itawapatia leseni ya uchimbaji wa Madini hayo.
Pamoja na mambo mengine Meneja huyo wa Mwamakiliga Gold Mining alibainisha kuwa miongoni mwa watu walionufaika na mgodi huo ni wakazi wa kijiji cha Mwamakiliga na kata ya Izunya Kwa ujumla ambao wamekuwa wakipewa kipaumbele katika nafasi mbalimbali za kazi zinazojitokeza katika mgodi huo.
" Sisi Kama Uongozi Wa mgodi huu tumeweka upendeleo maalum kwa wananchi wa kijiji hiki ambao ni wenyeji wetu, walinzi wengi wa mgodi wetu wanatoka hapa Kijiji cha Mwamakiliga, Pia tumechukua vijana 25 wa hapa kijijini na Kisha kuwafundisha kazi ya ukaguzi wa migodi vile vile wamiliki wa mashamba nao tunashirikiana nao vizuri Kwa vile wanakusanya asilimia zao kwaajili ya maendeleo yao na familia zao. ", alisisitiza Chitela.
Chitela alisema mbali na kuzalisha ajira hizo, mgodi wake umekuwa chanzo cha uhakika cha mapato ya halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale kupitia ushuru mbalimbali ikiwemo ushuru wa huduma.
Alisema kuwa hata serikali kuu imekuwa ikinufaika na uwepo wa mgodi huo kupitia malipo ya mrabaha, ambayo ni asilimia 3 kwa kila mifuko 100 ya mawe yenye dhahabu.
"Serikali imetuamini na kutukabidhi jukumu la kusimamia na kukusanya mapato yake katika mgodi huu, kazi hiyo tumekuwa tukiifanya kwa uaminifu mkubwa. Halmashauri yetu ya Nyang'hwale na serikali kuu wote wanapata mapato yao bila ubabaishaji", alibainisha Chitela.
Akizungumzia kuhusu usalama wa mgodi wake kwa wachimbaji na watu wengine wanaofanya kazi mgodini hapo, Chitela alisema kuwa suala la usalama kwao ni kipaumbele namba moja, na kwamba mgodi huo haujawahi kupata ajali yoyote kubwa kutokana na umakini wao mkubwa katika usalama.
"Mgodi wetu ni salama kabisa, kwetu suala la usalama ni kipaumbele cha kwanza na idara yetu ya ukaguzi ina watu wa kutosha na makini. Ukaguzi wa duara unafanyika wakati wote mchana na usiku, masaa 24 na mara ikibainila kama duara fulani ni hatarishi, tunasimamisha moja uchimbaji mpaka marekebisho yafanyike", alifafanua Chitela.
Kwa upande wake katibu msaidizi wa idara ya ukaguzi Chile Kishosha ameupongeza uongozi wa mgodi huo na serikali kwa ujumla kwa kuwawezesha yeye na vijana wenzake wavulana kwa wasichana kupata ajira ambazo mpaka sasa zinawasaidia kumudu maisha yao ya kila siku.
Hata hivyo Katibu mkuu Wa mgodi huo Doa Limbu anaishukuru sana serikali ya rais dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyotengeneza Mazingira mazuri Kwa wachimbaji wadogo, mgodi huo umezalisha ajira karibu makundi yote Vijana wanafanya shughuli ya uchimbaji Madini ya dhahabu lakini wengine wanafanya shughuli ya kubeba mawe kutoka maduarani kuyapeleka Sehemu sahihi kwaajili ya kukusanywa Kwa pamoja Ili badae yapelekwe kwenye Viwanda vya kuchenjulia lakini pia wenye mashamba tunapochimba Madini haya nao wananufaika kutokana na uwepo wa mgodi huo.
" Changamoto kubwa ni Miundombinu inayozunguka mgodi, mgodi huu upo mbugani, sisi kama mgodi mkakati wetu mkubwa tulionao ni mpango wa kudhibiti maji wakati wa mvua za masika kuanza manayake hili Eneo mvua zikianza changamoto ni kujaa maji, hivyo mpango wetu na mkakati wetu Kama ofisi ni kuja kuweka mitaro ambapo maji ya takuwa yanatoka huko juu kwenye milima yatapita kwenye mitaro na kuelekea mtoni," anasema katibu mtendaji wa mgodi Limbu.
Mary Abdala ambaye ni mhudumu wa ofisi Mwamakiliga Gold mine alishukuru kwa kupata kazi na kueleza kuwa kazi hiyo inamsaidia kuendesha maisha yake huku akisifu malipo anayopata kuwa yenye tija.
Nao wanufaika wengine WA mgodi huo Rebecca Marwa pamoja na Zaituni Mussa wakazi wa kijiji cha Khalumwa wilayani humo wanasema kuwa wanashukuru uwepo wa mgodi huo na umewasaidia kuweza kulwa familia zao pamoja na kumudu masomo ya watoto wao.


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)



